Mahitaji ya msingi kabla ya kuanza ufugaji wa samaki

Samaki ni nini?

Samaki ni mnyama mwenye damu baridi aishio majini (Anaweza kuwa na magamba au pasi na magamba). Nyama ya sasmaki imekuwa na mchango mkubwa sana katika lishe na chakula kiujumla. Samaki ni chanzo muhimu sana cha protini kwa binadamu na viumbe wengine. Nyama ya samaki ni nyama nyeupe ambayo husaidia kuondoa mazingira hatarishi ya kupata baadhi ya magonjwa yasiyo ambukizwa kama vile shinikizo la damu. Hivyo ulaji wa samaki ni muhimu kwaajili ya kuimarisha afya zetu.

Ufugaji wa samaki

Hii ni tasnia inayohusu uzalishaji na uhifadhi wa samaki kibiashara au kukidhi mahitaji ya nyumbani. Kutokana na ongezeko la watu kila siku, ni muhimu sana kujihusisha na tasnia hii kwa lengo la kuchochea upatikanaji wa nyama ya samaki na chakula kiujumla. Kiufupi şoko la samaki ni şoko la uhakika.

Unahitaji nini ili uanze kufuga samaki?

Eneo, Maji, Chakula, Vifaranga (mbegu), Soko.

Katika ukurasa ufuatao tutaangalia kila hitajio kwa kina.

Eneo

Katika ufugaji wa samaki, ni muhimu kuzingatia upatikanaji wa eneo litalotumika katika shughuli nzima ya ufugajİ. Zİngatİa yafuatayo wakatİ wa kuchagua eneo la kufugia samaki.

  • Udongo; Chagua eneo ambalo linahifadhi maji kwa muda mrefu ili kupunguza upotevu wa maji (udongo wa mfinyanzi unapendekezwa zaidi). Eneo lenye rutuba (mbolea) ni zuri zaidi kwaajili ya kuzalisha vyakula asilia ndani ya bwawa la samaki.
  • Maeneo yenye mafuriko; Epuka maeneo yote yenye historia za mafuriko ambayo huweza kupelekea upotevu wa samaki na hasara kubwa.
  • Mteremko; Epuka eneo lenye mteremko mkali, chagua eneo lenye mteremko kiasi au tambarale.
  • Uchafu; Epuka maeneo yanayofikiwa sana na uchafu kutoka sehemu nyingine. Mfano uchafu kutoka viwandani au maji taka.

Angalizo: Utazingatia yaliyotajwa hapo juu katika uchaguzi wa eneo kama unalengo la kufuga samaki kupitia mabwawa, kwa njia nyingine za ufugaji kama mfumo maji zungushi(RAS), si lazima kuzingatia mambo hayo wakati wa uchaguzi wa eneo la kufugia samaki.

Maji

Kwa sababu samaki ni viumbe wanaotegemea maji kwa kila kitu (Kuisha na kukidhi haja zote), Maji ni kipengele muhimu sana katika ufugajİ wa samakİ. Hİvyo hakikisha maji yanapatikana katika ubora na usalama. Maji ya mvua, bomba, mito, maziwa, na bahari yanaweza kutumika katika ufugaji wa samaki.

Ulinzi na usalama

Ulinzi na usalama; Kabla ya kuchagua eneo la kufugia samaki, zingatia usalama wa eneo hilo (Eneo likiwa karibu na nyumbani kwako ni zuri zaidi kwa sababu utahakikisha ulinzi na usalama.

Vifaranga vya samaki

Hakikisha unapata vifaranga bora vya samaki kutoka kwenye vyanzo au taasisi zinazoaminika kwa uzalishaji wa vifaranga vya samaki. Mfano; Big fısh farm, Miafo Company Limited au Sokoine University of Agriculture (ŞUA).

Epuka vifaranga vinavyotolewa kwenye mito au kutoka kwa wazalishaji wasioaminika kwani vinaweza kuwa chanzo cha kusambaza magonjwa na kupelekea udumavu. Wakati unaendelea na uwekezaji unaweza kuamua kuanza kuzalisha vifaranga vya samaki (mbegu) wewe mwenyewe na kudhibiti ubora wa vifaranga na kuwauzia wengine.

Aina za vifaranga vya samaki

  • Jinsia moja: Ufugaji wa samaki jinsia moja bila kuchanganya husaidia samaki kukuwa haraka. Hii ni kwa sababu samakİ jinsİa moja hawawezİ kuzaliana hivyo hakutakuwa na mashindano makubwa wakatİ wa kula chakula na nafasi ya makazi. Zaidi ni kuwa nguvu kubwa itaelekea katika ukuwaji na si kuzaliana. Mara nyingi watu hupenda kufuga madume tuu kwani hukuwa haraka na kuwa na uzito mkubwa zaidi ukilinganisha na majike.
  • Mchanganyiko: Samaki mchanganyiko (majike na madume kwa pamoja) huzaliana kwa kasi na kupelekea idadi ya samaki kuongezeka kwa kasi ndani ya bwawa la samaki. Ni jukumu la mfugaji kupunguza ongezeko la samaki, ili samaki wakuwe vizuri.

Chakula cha samaki

Ukuaji mzuri wa samaki unategemea sana ubora wa chakula kinachotumika. Kama chakula kinachotumika kina ubora mdogo, ni rahisi sana kupelekea udumavu wa samaki. Chakula bora ni chakula chenye mchanganyiko wa mahitaji yote ya ukuaji wa samaki (protini, nguvu, mafuta, vitamini na madini).

Masoko

Kama unafuga samaki kibiashara ni muhimu kuzingatia şoko la samaki wako. Katika hili inategemea pia na jamii ya samakİ unayofuga, mfano kama unafuga jamİİ ya şato şoko lake ni kubwa ukilinganisha na soko la kambale. Hİvyo, şoko la uhakika ni kipengele muhimu cha kuzingatia.

Miundombinu ya usafiri

Usafirishaji wa samaki kwenda kwenye masoko, usafirishaji wa chakula cha samaki, mbolea na vifaa vyote vinavyotumika katika ufugaji wa samaki hutegemea miundombinu ya usafiri. Hivyo eneo linalofikika kiurahisi zaidi na vyombo mbalimbali vya usafiri ni zuri zaidi kutumika.

Tamaduni mila na desturi

Zingatia miiko ya jamii inayokuzunguka (Mfano; kama jamii kubwa iliyokuzunguka haitumii samaki jamii ya kambale basi si vyema kufuga kambale katika eneo hilo)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *