Ufugaji wa samaki: Utangulizi

Ufugaji wa samaki ni kitengo cha uzalishaji kinachokuwa kwa kasi sana ulimwenguni. Hİİ İnatokana na upungufu mkubwa wa samakİ kutoka kwenye vyanzo asilia (mito, maziwa, bahari na mabwawa), hali inayopelekea ufugajİ wa samaki kuwa chanzo muhimu cha upatikanaji wa samaki. Uzalishaji huu unaweza kuchangia ongezeko kubwa la chakula na maendeleo ya uchumi kwa jamii yoyote na dunia kiujumla.

Ripoti zinaonyesha kuwa kuna ongezeko kubwa la idadi ya watu duniani. Hali hii inapelekea kuongezeka kwa uhitaji wa samaki mara dufu. Japokuwa ufugaji wa samaki unaweza kuchochea upatikanaji wa samaki kwa wingi, kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazorudisha nyuma tasnia hii ya ufugaji wa samaki.

Kitabu cha ufugaji wa samaki na taratibu zake, kitakupa muongozo na taratibu zote za kuzingatia katika ufugaji wa samaki kuanzia mwanzo wa ufugaji mpaka mavuno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *